TAMBUA
WEWE NI NANI KTK ULIMWENGU WA ROHO NA
MWILI!
Wakristo wengi siku hizi wanaishi
bila kutambua haki na wajibu wao kwa Mungu, hii imeleta shida kwenye wokovu wao hata wakaona kuwa wokovu ni mzigo.
shetani naye amewapofusha macho wasije wakajua siri ya uwezo na ukuu walionao.Je
wajua wewe ni nani?, Na una nafasi gani katika ulimwengu wa roho na mwili ?
unajionaje? Wewe ni mshindi au umeshindwa? Je wewe ni dhaifu au mzima? Wewe ni
masikini au tajiri? Neno linasema unavyojiona ndivyo utakavyokuwa- Mithali 23;7 unajitamkiaje? Unasema
wewe u nani? Neno linasema mtu anakula matunda ya kinywa chake -Mithali 18;20,21 acha kukuri vibaya
hata kama unajiona ni dhaifu sema mimi ni hodari Yoeli 3;10.Mara nyingine tunapotea kwa kutokuyajua maandiko wala
uweza wa Mungu.Yesu akawajibu, “Mwapotoka
kwa sababu hamjui maandiko wala uweza wa Mungu.Mathayo
22;29, Marko 12;24.
Hebu tuone sala ya Paulo kwetu Efeso
1;18-23.Kumbuka kila neno
lililoandikwa kwenye biblia ni kwa ajili yetu , Paulo anatuombea anasema;
“Ninaomba kwamba macho ya mioyo yenu
yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo: na
utajiri wa utukufu wa urithi wake katika
watakatifu jinsi ulivyo, na ubora wa
ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji
wa nguvu za uwezo wake: aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu,
akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme
wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si
ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akivitia vitu vyote chini ya
miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Maneno haya yanatuambia kwamba Kristo
alifufuka na kukalia kiti cha enzi cha Mungu., Je, wajua kwamba unatawala pamoja naye katika huo ulimwengu wa roho?
Paulo anathibitisha jambo hili katika ufasaha kwenye maandiko mengine
mawili: “akatufufua pamoja naye, katuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa
roho, katika Kristo Yesu” (Waefeso
2:6); “na ninyimmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na
mamlaka” (Wakolosai 2:10).
Nataka
nikukumbushe mambo ambayo bibilia imesema kutuhusu kuwa sisi ni nani? Kisha
Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno Yangu,
mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka
huru.’’Yoh 8 31, 32. Hapo sina la
kuongezea lakini naamini umejua kuwa kweli (neno) ikilijua linakuweka huru.
Bwana Yesu asifiwe!.
MAMBO YANAYOTUTAMBULISHA.
Ø WEWE NI UZAO MTEULE;.
Je unajua hilo
“sema mimi ni uzao mteule” Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda
kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini
Mimi nimewachagua kutoka katika
ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. Yoh 15;19
Si ninyi
mlionichagua, bali Mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae
matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika
Jina Langu, awape.Yoh 15;16
Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa
ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake
ya ajabu. Mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni taifa la Mungu.
Mwanzo mlikuwa hamkupata rehema, lakini sansa mmepata rehema. 1pet 2;9.
Kwa maana
alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana
Wake mpendwa,
kol 1;13.
Kwa hiyo sisi tumehamishwa
kutoka kwenye mambo ya dunia na kuingizwa katika ufalme au uraia mwingine (
katika ulimwengu war oho), japo bado tunaishi duniani lakini wenyeji wetu ni
mbinguni, sawasawa na mtu anayeishi Malawi lakini ni mwenyeji wa Tanzania
haimaanishi yeye ni mmalawi. Kwahiyo
usizifuate tabia za wamalawi yafikirini yaliyo juu siyo chini. Amen.
Ikiwa
umeokoka, tembea ukijua wewe ni tofauti na wengine na si lazima ufanye kila
linalofanywa na wengine maana mengine si yanyoruhusiwa kwenye utaifa au uraia wako!,
na kwa kufanya hivyo ulimwengu utakuchukia ,sisemi ujivune au ujibague bali ujue kuwa kuna mambo ambayo watu wengine
watafanya lakini wewe hutafanya maana una “speed governor” inayokuongoza na hii
yamkini itasababisha ulimwengu kukuchukia! Take care, weka moja kichwani!!.
Ø
WEWE NI
MTAKATIFU;
“sema mimi ni
mtakatifu’ mtakuwa watakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu Lawi 19;2 mahali pengine anasema mtakuwa wakamilifu maana mimi ni
mkamilifu pia biblia inasema katika zaburi- watakatifu waliopo duniani ndio
ninao pendezwa nao.Pokea ahadi hiyo ni yako jua unayezungumziwa ni wewe mototo
wa mungu usione hili neno aliyeandikiwa nimwingine, ni wewe mwenyewe. Kama
unaamini kuwa una roho mtakatifu basi pia amini kuwa wewe ni mtakatifu kwa
sababu roho mtakatifu hakai mahali palipo pachafu. Kwa habari ya Watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao
ninapendezwa nao. Zab 16;3 kama
wewe hutaki kujikubali kuna watu Mungu anawakubali na unavyo jiona ndivyo
utakavyo kuwa kumbuka hilo pia. Kwa hiyo iweni wakamilifu kama Baba yenu
wa mbinguni alivyo mkamilifu.’’Mathayo
5;48. Mpendwa umeshakombolewa na kusafishwa kwa damu yake ambayo
haikumwagika bure bali ni kwa kututakasa . Katika
Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu Yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa
na wingi wa neema Yake Efeso1;7,4.
Ø WEWE NI MWANA AU MTOTO WA MUNGU;
Wewe
si mtu wa Mungu bali u mwana! “sema
nimefanyika kuwa mwana na nimehesabiwa haki”. Bali wote waliompokea,
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake.
Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya
mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu. Yoh 1;12
Naamini na wewe unafanya hivyo yaani ulimpokea na unaamini,basi umefanyika
kuwa mwana na kama ujuavyo mtoto wa kondoo ni kondoo, na mwana wa Mungu ni
mungu mdogo!Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu
watoto wa Mungu. Basi ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi,
warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja Naye tupate
pia kutukuzwa pamoja .Rum 8;16 sisi
warithi wa Mungu walithio pamoja na Kristo,kwa hiyo sisi sio watoto wa kambo
kwa Mungu bali ni wana na ndio maana ni warithi pamoja na Kristo maana mtoto
hana fursa ya kurithi.
Kwa kuwa
wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio watoto wa Mungu.Rum 8;14 Je wewe
unaongozwa na roho? Kama ni jibu ni ndiyo-safi! maana wewe ni mwana wa Mungu.
Kila
mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu na ye yote ampendaye
Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.Hivi ndivyo tunavyojua kwamba
tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri Zake.Kwa kuwa
huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito.Kwa
maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kuushinda
kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.Ni nani yule aushindaye
ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.1yoh 5;1-4
Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba
sisi tuitwe watoto wa Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini ulimwengu
haututambui, ni kwa kuwa haukumtambua Yeye. 1yoh 3;1
Ninyi ni rafiki
Zangu mkifanya ninayowaamuru. Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu
watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana
nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba Yangu.Yoh 15;14,15. Kwa hiyo kwetu Yesu ni
Baba pia ni rafiki.
Ø WE NI KUHANI NA MFALME ;
“
Sema mimi ni kuhani tena ni mfalme”unajua
kazi ya kuhani namfalme? Najua unajua lakini makuhani enzi hizo ni watu ambao
ndio tu waliokuwa wakirusiwa kuingia patakatifu lakini sasa nasi tumefanyika
kuwa makuhani tunapaingia patakatifu kwa damu ya Yesu! Ufunuo 5;10 ,1;6 lakini kama ujuavyo mfalme ni mtu mwenye mamlaka,
hatutegemei mfame akiomba bali
anaamuru Bwana Yesu asifiwe!.Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia
Mungu wetu, nao watamiliki katika
dunia.’’ Ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa
takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli. Kutoka19;6 . Nabii Isaya alikuwa ameona akasema, Nanyi mtaitwa
makuhani wa BWANA,mtaitwa watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, nanyi katika
utajiri wao mtajisifu.Isaya 61 ;6
Ø WEWE NI KIUMBE KIPYA;
Ya kale yote yamepita, iambie nafsi yako mimi ni kiumbe kipya! 2kor 5;17
Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa
kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. Kwa hiyo kuwa
huru kwa mambo yaliyopita usikumbuke Misri wala usitamani nyama za Misri hata
kama kuna dhambi kubwa ulitenda jua Mungu haikumbuki maana amesema uovu wenu
sitaukumbuka kamwe kwa hiyo hajui dhambi uliyotenda na anakushangaa. Anasema
dhambi zenu zitakuwa nyeupe. Nimesulibiwa
pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi bali Kristo ndiye aishiye ndani
yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu,
aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu Gal 2;20.
Ø UMEBARIKIWA PAMOJA NA IBRAHIMU!
Sema
hivyo ili ule matunda ya midomo yako Gal3;9
Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini
wanabarikiwa pamoja na Abrahamu, mtu wa imani. Hiii ni kwa sababu wewe
unaamini kama Ibrahimu aliyekuwa akimwamini Mungu. Rum8;17 Basi ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa
Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja Naye tupate pia
kutukuzwa pamoja Naye.
Kwa hiyo, ahadi
huja kwa njia ya imani, ili iwe ni kwa neema na itolewe kwa wazao wa Abrahamu,
si kwa wale walio wa sheria peke yao bali pia kwa wale walio wa imani ya
Abrahamu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote. Rum
4;16 kwa hiyo lazima uamini na kuipokea ahadi hiyo ndipo itakuwa yako~maana
anasema ahadi huja kwa njia ya Imani.
Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, nawe
ikiwa ni mtoto, basi wewe pia ni mrithi, mrithi wa Mungu. Gal 4;7
Ø UWEZO WA YESU NI UWEZO WAKO!
Sema
nayaweza mambo yooote katika Yeye anitiayanguvu Fil 4;13
Nanyi
ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu
kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa
wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani
yenu.
.Rum 8;11
Yoh 14;12 Amin, amin,
nawaambia, ye yote aniaminiye Mimi, kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa sababu
Mimi ninakwenda kwa Baba.Efeso 1;20 na
uweza Wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo
unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno Mungu alitufufua pamoja
na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu,Efeso 2;6
Ahimidiwe Mungu
na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo. Efeso 1;3 hizi ni Baraka za rohoni
ambazo ni kubwa kuliko zile za mwilini
ukiwa nazo hata kimwili umefanikiwa 3yoh
1;2 .13Tunajua kwamba twakaa ndani Yake na Yeye ndani yetu, kwa
sababu ametupatia sisi sehemu ya Roho Wake. 1yoh 5;13
Ø WEWE UNA MAMLAKA;
“Nina mamlaka” Mathayo
16;19 Yesu
akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya
magonjwa yote, kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya
wagonjwa. Luka 9;1
Kwa
kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale
uliompa. 3Nao Yoh 17;2
Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na
ng’e na juu ya nguvu zote za adui, wala hakuna kitu cho chote kitakachowadhuru
kwa namna yo yote.Luka 10;19
Ø WEWE NI MSHINDI;
Washindi Bwana
Yesu asifiwe!
Rum 6;14 1yoh 5;18 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili
wake, juu ya mti, ili kwamba,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi
katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa.1pet2;24
Nanyi ikiwa Roho wa
Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua
Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya
Roho Wake akaaye ndani yenu. Rum 8;11
Lakini ninyi,
hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu
ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. Lakini kama Kristo
anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi
hai kwa sababu ya haki.Rum 8;9 na
kwasababu Yesu alishinda kwa habari ya dhambi na mauti nasi vivyo hivyo nasi ni
washindi kwani tunamwamini mshindi nay eye yuko ndani yetu!
Ø WEWE UNA UUNGU NDANI YAKO;
Rum
8;29 Nanyi ikiwa Roho wa
Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua
Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya
Roho Wake akaaye ndani yenu. Rum 8;11
roho wa Mungu anakaa ndani yetu.
Uweza Wake wa uungu umetupatia mambo yote
tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua Yeye aliyetuita
kwa utukufu Wake na wema Wake mwenyewe 2pet
1;3 Kisha BWANA akamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa
Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. Kutoka 7;1
Ø WEWE NI NURU NA CHUMVI PIA;
Mathayo 5;14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu.
Yoh
8;12Kwa
maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote,
haki na kweli,) nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki matendo ya
giza yasiyofaa, bali yafichueni. Efeso 5;8-11. ‘‘Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake,
yawezaje kurudishiwa ladha yake tena ? Haifai tena kwa kitu cho chote, ila
kutupwa nje ikanyagwe na watu. Math 5;13
Ø WEWE NI TAJIRI;
2kor 8;9 Kwa
maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa
ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili
kwa umaskini Wake ninyi mpate kuwa matajiri.
kol 1;13 1yoh 4;43 Ikiwa
Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa
ukarimu pamoja Naye? Rum 8;32 Hivyo basi, mtu asijivune kuhusu wanadamu!
Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu, ikiwa
ni Paulo au Apolo au Kefa au dunia au uzima au mauti, au wakati uliopo au
wakati ujao, haya yote ni yenu na ninyi ni wa Kristo, naye Kristo ni wa Mungu. 1kor 3;21-23
Ø
WEWE NI
HEKALU,KIUNGO NA TAWI;
Je, hamjui ya kwamba ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho
wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu ye yote akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu
atamwangamiza mtu huyo, Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu,
ambalo ndilo
ninyi.1kor 3;16 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo? 1kor 6;15. Miili yetu ni hekalu na si
hekalu letu sisi bali ni la roho mtakatifu na tumeazimwa tu, bali tuifanyie
kazi vizuri ili mmiliki (roho mtakatifu) afurahi siku zote!.Mahali pengine
anasema mimi ni mzabibu nanyi ni matawi.
Ø
WEWE NI RUNGU LA
BWANA LA VITA;
Mungu anasema
kuwa wewe ni Silaha yangu ya vita kwa
wewe navunjavunja mataifa,kwa wewe naangamiza falme, kwa wewe navunjavunja
farasi na mpanda farasi, kwa wewe navunjavunja gari la vita na mwendeshaji
wake, kwa wewe napondaponda mwanaume na mwanamke, kwa wewe napondaponda mzee na kijana, kwa wewe napondaponda kijana wa kiume na mwanamwali, kwa wewe nampondaponda mchungaji na kundi, kwa wewe nampondaponda mkulima na
maksai, kwa wewe nawapondaponda watawala na maafisa. “Mbele ya macho yako
nitamlipiza Babeli na wote waishio Ukaldayo kwa ajili ya makosa yote
waliyofanya katika Sayuni,’’ asema BWANA.Yer
51;20-24
v
KUKIRI
Baba Mungu mfalme wa wafalme uketie mahali pa juu
palipo inuka sana, asante kwa neno lako lililonifikia leo ili kunijulisha na
kunikumbusha nafasi yangu ! Neno lako linasema nitakula matunda ya midomo yangu
nami najitamkia na najitambua kuwa mimi ni uzao mteule,mimi ni mtakatifu, mimi
ni tajiri,mimi ni mzima,mimi ni mshindi,mimi ni rungu lako Bwana,mimi ni chumvi
na Nuru ya kuwaangazia wengine,mimi ni mshindi na nina mamlaka, mimi ni kuhani
na mfalme katika jina la Yesu Kristo Mungu nisaidie kutembea na kujua mimi ni
nani na nafasi yangu niitumie ipasavyo katika Jina la Yesu kristo nimeomba.
Amen!
HAYA NI BAADHI TU
YA MAMBO MENGI TULIYOANDIKIWA KWENYE BIBLIA~ILI KUELEWA ZAIDI MAMBO HAYA NA
NAFASI YAKO NAKUSHAURI UANZE KWA KUSOMA KITABU CHA WAEFESO HUKU UKIMWOMBA ROHO
MTAKATIFU AKUSAIDIE ZAIDI ILI UPATE KUELEWA! MUNGU AKUONGOZE NA
AKUBARIKI SANA! AMEN!
Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa
njia ya Roho Wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu
1kor 2;10
ü 0756688789
ü SEME FREDY .A.
Amen ubarikiwe sana mtu wa Mungu
JibuFuta