Jumatano, 8 Oktoba 2014

KILA JAMBO LINA KUSUDI-TAFAKARI HILI!
Kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume 16;16-40.
        16Siku moja, tulipokuwa tukienda mahali pa kusalia, tulikutana na mtumwa mmoja wa kike ambaye alikuwa na pepo wa uaguzi naye alikuwa amewapatia mabwana zake mapato makubwa ya fedha kwa ubashiri. 17Huyu mtumwa wa kike alikuwa akimfuata Paulo na sisi akipiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, wao wanawatangazieni njia ya wokovu.” 18Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo akamtoka saa ile ile.
19Basi mabwana wa yule mtumwa wa kike walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta mpaka sokoni mbele ya viongozi wa mji. 20Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi. 21Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Kirumi hatuwezi kuzikubali au kuzitimiza.”
22Umati wa watu waliokuwepo wakajiunga katika kuwashambulia na wale mahakimu wakawaamuru wavuliwe nguo zao wakatoa amri Paulo na Sila wachapwe viboko. 23Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu, 24kwa kufuata maelekezo haya, yule mkuu wa gereza akawaweka katika chumba cha ndani sana mle gerezani na akawafunga miguu yao kwa minyororo.
25Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka. 27Yule mkuu wa gereza alipoamka na kuona milango ya gereza iko wazi, akachomoa upanga wake akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wote wametoroka. 28Lakini Paulo akapiga kelele kwa sauti kubwa, akasema, “Usijidhuru kwa maana sisi sote tuko hapa!”
29Yule askari wa gereza akaagiza taa ziletwe, akaingia ndani ya kile chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka mbele ya Paulo na Sila. 30Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini ili nipata kuokoka?”
31Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na wa nyumbani mwako.” 32Wakamwaambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. 33Wakati ule ule yule mkuu wa gereza akawachukua akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa. 34Akawapandisha nyumbani mwake akawaandalia meza mbele yao, yeye pamoja na wa nyumbani mwake wote wakafurahi sana kwa kuwa amemwamini Mungu.
35Kulipopambazuka wale mahakimu wakawatuma maafisa wao kwa mkuu wa gereza wakiwa na agizo linalosema, “wafungue wale watu, waache waende zao.” 36“Mahakimu wametuma niwaache huru, kwa hiyo tokeni.”
37Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raia wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Kweli hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.”
38Wale maafisa wakarudi na kuwaambia wale mahakimu maneno haya, wakaogopa sana walipofahamu kuwa Paulo na Sila ni raia wa Rumi. 39Kwa hiyo wakaja wakawaomba msamaha, wakawatoa gerezani, wakawaomba waondoke katika ule mji. 40Baada ya Paulo na Sila kutoka gerezani walikwenda nyumbani kwa Lidia, ambapo walikutana na wale ndugu walioamini, wakawatia moyo, ndipo wakaondoka.
KATIKA MAANDIKO HAYA TUNAJIFUNZA YAFUATAYO;
1.Maisha ya maombi;
Ø  Mstari wa 16; “Siku moja, tulipokuwa tukienda mahali pa kusalia” ina maana ilikuwa ni desturi yao kusali ndio maana mahali pao pa kusalia palikuwa panafahamika.tujifunze kutokana nao tusiacha kukusanyika kila itwaapo leo! Soma  Ebrania 10;25.
2.Unaweza ukawa unampatia faida mtu au shetani kwa kujua ama kutokujua.(yaani sheani kukutumikisha na kujipatia faida kupitia wewe).
Mstari wa 16 “tulikutana na mtumwa mmoja wa kike ambaye alikuwa na pepo wa uaguzi naye alikuwa amewapatia mabwana zake mapato makubwa ya fedha kwa ubashiri”.Biblia hajaweka wazi kama yule mama alikuwa anajielewa kuwa anatumika kuwapatia faida mabwana zake au la na pia kwenye hiyo faida iliyokuwa ikipatikana alikuwa na fungu lake au la na vitu kama hivyo!
Pia unavyoenda kwa waganga ni kwamba shetani amekuweka wewe kuwa kitega uchumi wewe ni mradi kwa waganga maana unavyowapatia fedha unawapatia faida na hawawezi kukupa Amani watakupa utulivu tu. Maana hutapona na hatimaye utakuwa “dependant” kwao.Achana nao!
3.Si kila anayekusifia au kukunadi ana roho nzuri.
Ø  Mstari wa 17 Huyu mtumwa wa kike alikuwa akimfuata Paulo na sisi akipiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, wao wanawatangazieni njia ya wokovu.” Ukiangalia maneno aliyokuwa akiyasema yule mwanamke ni mazuri tu! Hayana matusi wala si ya kipuuzi lakini……yahitaji macho ya roho kuyajua haya!. kwa hiyo mpenzi msomaji wangu shetani anaweza kukupumbaza kwa sifa fulani lakini tunahitaji hekima na Roho Mtakatifu kuzitambua kila hila za mwovu kama Paulo alivyotambua ile roho chafu.
4.Kuzitambua roho.
Ø  Mstari wa 18“lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo akamtoka saa ile ile. Ok kwanini Paulo audhike au asikitike kama yule si roho mchafu?. Ukisoma Biblia nyingine ianasema Paulo akasikitika.Mimi naweza kusema alikosa Amani,kwa hiyo kama kuja jambo linafanyika nawe unakosa Amani au unasikitika au unaudhika ujue hakuna usalama hapo.Kwa hiyo unaweza kukemea kama Paulo au hata kimoyomoyo na uataona matokeo.
5.Nguvu za jina la Yesu na mamlaka ndani yako.
Ø  Mstari wa 18. “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!”.Tumia jina la Yesu maana lina nguvu,ya kuzishinda nguvu zote za giza pia umepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka.Na nguvu yoyote ya giza lazima itii mara si kubembeleza pepo kwa muda mrefu,hiyo ni shida ambayo lazima tuepuke,maana biblia inasema “Yule pepo akamtoka saa ile ile”lakini kwa namna nyingine tunaweza tukasema akamtoka dakika ile ile au sekunde ile ile.
6.Unapofanya “impact” kweli ulimwengu wa giza tegemea vita “either” kimwili au kiroho.
Ø  Mstari wa 19 “Basi mabwana wa yule mtumwa wa kike walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta mpaka sokoni mbele ya viongozi wa mji.”Hizi tunaweza kuita roho za malipizi na visasi maana shetani anakuwa hajafurahi.Nuru ikiingia giza hukimbia tena huchukia. Zikija huna budi ya kuendelea kusimama imara maana mwingine anaweza kunung’unika kuwa nimefanya kazi ya Mungu lakini bado yamenipata! Kwanini?........kwanini Mungu ameniacha?......hapana Mungu bado yuko nawe hajakuacha. Ila “LIPO KUSUDI KWA HAYO UNAYOPITIA”.Hivyo endelea kumtegemea Mungu,kuomba msaada wake kwa hayo na ulinzi wake.
7.Unaweza kuzushiwa kwa mambo yasiyokuwa kweli.
Ø  Mstari wa 20 Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi. 21Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Kirumi hatuwezi kuzikubali au kuzitimiza.”Ki-ukweli akina Paulo hawakuleta ghasia nao walikuwa si wayahudi maana mstari wa 38 “Wale maafisa wakarudi na kuwaambia wale mahakimu maneno haya, wakaogopa sana walipofahamu kuwa Paulo na Sila ni raia wa Rumi”. Tena unaweza kudhalilishwa lakini bila kosa mstari 22 “Umati wa watu waliokuwepo wakajiunga katika kuwashambulia na wale mahakimu wakawaamuru wavuliwe nguo zao wakatoa amri Paulo na Sila wachapwe viboko”.
8. Siyo kila aliyeko jela ana hatia.
Ø  Mstari wa 23.Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu.ukweli walikuwa hawana hatia, hata kama huko gerezani walipata nafasi ya kuulizana kuwa “imekuwaje ndugu umefika hapa?”wafungwa wangesema tuliiba,tuliua,tulibaka,tulikwapua simu…..n.k bali wao wangesema ni Yesu tu.ehee ni Yesu?.........ki vipi yaani? Ndipo wangesema,Tulimtoa mwanamke mmoja pepo kwa jina la Yesu ndio maana tuko hapa…….! Haa! Mbona hilo halipo kwenye sharia wali si kosa bali ni jambo jema(wangeshangaa). Tena akina Paulo walihukumiwa Zaidi ya wale wengine maana mstari wa 23 “Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu, 24kwa kufuata maelekezo haya, yule mkuu wa gereza akawaweka katika chumba cha ndani sana mle gerezani na akawafunga miguu yao kwa minyororo”
9.Nguvu ya maombi na kusifu.
Ø  Mungu ameketi katika sifa kwa hiyo unaposifu unakuwa ume “put on button”ya Mungu kuonekana kwako na akionekana lazima wewe uguswe tu kwa namna yoyote.Soma mstari 25 “Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka”.
9.Njia ya wokovu ni kumwamini Yesu Kristo.
Ø  Yule mkuu wa gereza aliuliza mstari wa 30 Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini ili nipata kuokoka?” nao wakamjibu mstari 31Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na wa nyumbani mwako.”soma pia Warumi 10;9-10.
10. Mungu akikuokoa anakuokao wewe na nyumba yako.
Ø  Nao wakamjibu mstari 31 “Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na wa nyumbani mwako”.kwa hiyo kama Mungu amekupa neema ya wokovu muombe pia aokoe na ndugu zako pia, ni raha sana!

KINGINE TUNACHOJIFUNZA KATIKA MAANDIKO HAYA.
Ø  Usiwaombee mabaya wanaokuudhi bali waombee mema.Hatujasoma wala kuona kama akina Paulo waliwalaani au kuawaombea mabaya wale mabwana na makadhi.
Ø  Ukilibeba jina la Yesu jiandae kwa mapambano na vita,lakini ushindi upo kwa tunashinda na Zaidi ya kushinda kwa Yeye atutiaye Nguvu na akiwa upande wetu na aweza kuwa juu yetu?........
Ø  Si roho zote zinazomkiri Mungu zinatoka kwake,unaweza kuzijua kwa kukemea kama Paulo alivyofanya,unaweza kukemea hata kimoyo moyo na utaona matokeo yake,lakini hata kabla hujakemea utaona kuwa unakosa Amani.
Ø  KILA KITU KINA KUSUDI LAKE.Hapa tunaona watu wakihubiriwa,pepo wakitoka,mkuu wa gereza aokoka na nyumba yake, Zaidi Mungu anatukuzwa.

NAMUOMBA ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE ZAIDI KUTAFAKARI HAYA!. MUNGU AKUBARIKI TUONANE KWA MARA NYINGINE WAKATI MWINGINE………………………………………AMENI!..................................................................................................

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni