UMUHIMU WA KUMSHUKURU
MUNGU KWA KILA JAMBO; EFESO 5;20.
Namshukuru Mungu kwa kutufikisha
mpaka siku na masaa machache yamwaka huu(2014)
zimebaki siku saba(7) tu sawa sawa na masaa (168 )mia moja na arobaini na nane ,ili
tuumalize mwaka huu(2014) na tuingie mwaka 2015, hii ni neema,haleluya!.Ukitaka
uishi kwa furaha na amani na upate
sababu zaidi za kumshukuru Mungu,tafakari yale tu Mungu aliyokutendea wewe
kwanza wala usijilinganishe na mwingine kwa maana kila mtu Mungu ameipanga ratiba
au plani ya masha yake .
Leo nataka tukumbushane umuhimu
wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.kila mtu kuna vitu ambavyo amepitia vinaweza
vikawa vizuri au vibaya au vyote kwa pamoja lakini sababu ya kumshukuru Mungu
ipo kwa hali hizo zote haijalishi. Mungu anasema “Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye
aiandaaye njia yake jinsi ipasavyo nitamwonyesha wokovu wa Mungu.’’(zaburi
50;23).Tumshuru Mungu na maandalio ya mioyo yetu yawe katika mtazamo wa
kumtegemea Mungu kwa mwaka mwaka ujao.
Tunapaswa kumshukuru na kumtukuza Mungu
kwa kila jambo liwe lenye furaha au amani. Maana huwezi ukajua unachoona ni
kibaya kumbe kwa Mungu ni kizuri na ana mipango mizuri na wewe! Huwezi ukajua
kuwa mungu amekupigania kwa kiwango gani au namna gani, na badala ya kutokia
hicho kilichotokea pengine kingitokea
kibaya zaidi ya hicho.kwahiyo tunachopaswa ni kushukuru na kumsifu mungu hajalishi umepitia katika
mambo mazito na magumu kiasi gani lakini
mungu alikuwa na plan ana mpango na maisha yako kwahiyo si vabaya ukamshukuru Mungu
kwa namna zozote unaoona zinafaa.. Paulo anasema “sikuzote mkimshukuru Mungu Baba katika Jina
la Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila jambo.(Efeso 5;20)
Mimi nimejifunza kumshukuru Mungu na
kumtukuza Mungu hata kwenye wakati mgumu na katika mambo yanayoudhi na kusikitisha
na haya niliamua kuyweka kwenye matendo, yaani kila nilipo pata kitu Mungu alinikumbusha kumwambia asante,
nikifanya hivyo napata amani na ndipo
nilijua hakika Mungu anatupenda sana haijalishi ni mambo gani tunayopitia.kwa kifupi
unapomshukuru mungu kwa kila jambo unapata yafuatayo;
I.
Amani ; unapoenda mbele za Mungu na
kusema “Mungu nakushukuru kwa yote na ninakutukuza” unapata amani kwa maana umesalenda kwa Mungu
na huo mzigo uliokuwa nao unakuwa umemtwika Mungu(1peto 5;6). Mfano umepata
hasara ya mradi wako unapomshukuru Mungu na kumtukuza kwa moyo wako wote
unapata amani maana pia unakuwa umejinyenyekeza
hata kama ulikuwa na uchungu uanaisha unapata amni ya Kristo. Liweke hili katika matendo hili ili ujue nini namaanisha.
II.
Unapata majibu; mungu anaweza kukuambia
kuwa mwanangu nimeliruhusu hili litokee au likupate kwa sababu……..kwa hiyo bado
unakuwa ujua kinachoendelea ktk maisha yako na hii itakupa ujasiri. Lakini
usipopata muda wa kushukuru huwezi ukajua chochote zaidi utaumia,utachanyikiwa
na mbaya zaidi utaanza kulalamika.
III.
Mungu anajivunia wewe maana hata katika shida pia kuna sifa mbele
za Mungu ni kama Paulo na sila gerezani (Matendo 16;25), sifa zao kwa Mungu
hazikuzima,ni kama ayubu hakuacha kumshukuru Mungu pamoja na shida zake.Sasa
hapo shetani anasema huyu simwezi tena maana nilijua hapa ndipo atakapo tamaa
lakini ndo sifa zake zimekuwa za juu mbele za Mungu wake. Na mungu anatabasamu
anasema hakika mwanangu amenijua.
IV.
Kiwango chako cha imani kinapanda; kadri
unapopitia magumu na majaribu ya kuvunja
moyo, ndipo imani yako huongezeka. Pia hiyo ni gia ya kusonga mbele maana ukishinda unarudia ukiweza unasonga mbele zaidi
(Yakobo 1;2-3 Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na
majaribu mbalimbali, kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta
saburi.
V.
Unapomshukuru na kumsifu Mungu wakati wa
shida unavuka eneo la kulalamika na ambalo ni baya sana maana najua unakumbuka kilichowapata wanawa Esraeli
walipokuwa wakilalamika.
Haya
ni baadhi tu ya mengi lakini tumuombe Mungu atupe moyo wala shukurani atuepushe
na kulalamika.
Ningipenda kusema pia kuwa ;usithubutu kumuacha
Mungu kwa chochote au kwa lolote bali acho chochote au lolote kwa ajili ya Bwana
Anza
na Bwana;maliza na Bwana anayeanza na kumaliza na Bwana hufanya vema sana
nakutakia mwisho mwema wa mwaka 2014 na mwanzo mwema wa mwaka 2015, kwa
kila jambo utakalo lifanya mwaka 2015, Mungu akatangulie mbele yako, liliogumu
likawe jepesi katika jina la Yesu uliposhindwa mwaka 2014, mwaka 2015 ukashinde
nakutangazaia ushindi wako kwa mwaka 2015 katika jina la Yesu. Mungu akahusike
na siku zote 366(mia tatu sitini na sita) zilizoko ndani ya mwaka!, miezi yote
12( kumi na mbili ) ya mwaka ,wiki zote za mwaka siku zote za mwaka ,masaa,
dakika na hali kadhalika sekunde. Mungu akawe pamoja nawe na Roho wake
akakuongoze katika Jina la Yesu Kristo jina lenye nguvu lipitalo majina yote
ameni.!
Nakutakia
heri ya Krisimasi na mwaka Mpya. Wewe umebarikiwa!